eBUSINESS - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

eBUSINESS

Fahamu maana ya biashara kwa njia ya intaneti (E-Commerce)
Je, umekuwa ukijiuliza nini maana halisi ya kufanya biashara na kupata kipato kupitia intaneti? Au pengine ulikuwa ukijiuliza maswali mengi kuwa unaanzaje kuuza au kununua kwenye intaneti? Hapa utajifunza na kufahamu maana halisi ya eCommerce na jinsi inavyofanya kazi. Mwisho wa siku utakuwa muuzaji au mnunuaji kupitia intaneti. Na kwa maana hiyo utakuwa miongoni mwa mamilioni ya watu ambao wamekamata fursa za kibiashara kutumia intaneti.
Maana ya eCmommerce ni kitendo cha kuuza au kununua bidhaa na/au huduma kwa njia ya intaneti. Shughuli hii ilianza miaka ya 1960 baada ya kuibuka teknolojia iitwayo Electronic Data Interchange (EDI) ambapo mfumo huo uliwezesha makampuni au watu kuweza kubadilishana hati, hundi au risiti za kibiashara kwa kutumia komputa zilizounganishwa na intaneti.
Shughuli hiyo ilishika kasi zaidi kufikia miaka ya 1990 na mwanzo wa mwaka 2000. Mfano mwaka 1994, kampuni ya Dell Incorporation ya Texas Marekani ilianzisha tovuti au mtandao wa dell na hadi mwaka 1999 kiwango cha mauzo kilipanda sana kulingana na fursa aliyopewa mteja kuweza kununua hata kifaa kimoja kimoja cha komputa yake. Mwaka 1995, mtandao wa Amazon ambao makao yake makuu yapo Seattle, Washington Marekani ulianzishwa na mmarekani mmoja aitwaye Jeffrey Preston Jorgensen "Jeff Bezzo" kwa madhumuni ya kuuza vitabu. Mwaka huohuo mtandao wa ebay ulianzishwa na mtaalamu wa mambo ya programu za computer aitwaye Pierre Omidyar ukitoa uwezo wa mtu kuuza bidhaa kwa mtu mwingine. Mwaka 1999 soko la alibaba lilianzishwa nchini China. Soko la alibaba kwa sasa ndio linaongoza kwa ukubwa duniani kwa maana ya kuwa na wauzaji na bidhaa nyingi pia wanunuzi wengi. Kwa ujumla mitandao yote hiyo imekua sana kulingana na ongezeko la wadau kutoka duniani kote.
Makundi makuu ya eCommerce
B2B (Business to Business)
Ni mfumo wa biashara unaohusisha wenye viwanda wakiwauzia wafanya biashara wakubwa wanaouza kwa jumla au kiwanda kwa kiwanda wakiuziana au mfanya biashara wa jumla akimuuzia mfanya biashara mwingine auzaye kwa jumla. Mfano wa masoko hayo ya B2B ni kama alibaba.com, made-in-china.com, globalsources.com, tradett.com na mengine mengi.
Habari njema ni kwamba hata wewe mnunuaji wa kawaida kama unataka kununua bidhaa moja kutoka B2B inawezekana hasa kwa alibaba.com. Cha kufanya wakati unataka kununua nwambie muuzaji kuwa unanunua sampuli (commercial sample), hapo unaweza kununua hata memory card moja ya Mb128 na watakutumia. Nisemapo memory card ya mb128 sitanii, mimi mwenyewe nimewahi kununua hivyo. Moja ya sababu za maendeleo waliyoyapata wachina ni pamoja na uwezo wao wa kuuza bidhaa kuanzia moja kwa bei yoyote na wako tayari kukuhudumia sawa na anayenunua bidhaa za kujaa kontena la futi 40.
C2C (Consumer to Consumer)
Huu ni mfumo wa kibiashara ya intaneti ambao unahusisha mtu na mtu wakiuziana bidhaa moja au zaidi. Hapa unaweza kuuza au kununua bidhaa ya aina yoyote hata kama ni ndogo na kwa thamani ndogo. Mfano wa masoko haya ni kama aliexpress.com, ebay.com, craiglist.com, etsy.com na mengine mengi.
B2C (Business to Consumer)
Kundi hili linahusisha wauzaji wakubwa au viwanda kuwauzia makundi ya wateja aina zote. Hapa pia hutumika mifumo ambayo hakuna mtu katikati wa kuweza kumwuliza (hadi ikibidi) kwani kila kitu unakuta kimewekwa bayana na hiyo mifumo kwa maana ya muundo wa hiyo bidhaa (specifications/descriptions), bei hadi ulipo (CIF), mzigo unatumwaje na shirika gani na unaweza kuchagua shirika gani ulitumie kusafirisha na bei zake, kwa hiyo unakuta kila kitu kimewekwa na hiyo mifumo hivyo huna haja ya kuuliza mtu. Mfano amazon.com, ebay.com, aliexpress.com na masoko mengine.
C2B (Consumer to Business)
Hapa unakuta mtu binafsi (end user/consumer) anaweka bidhaa yake au huduma kwa njia ya mnada, kisha makampuni yanashindana dau. Baadae huyu muuzaji binafsi anachagua kampuni gani aiuzie hiyo bidhaa au huduma. Mfano wake ni kama elance.com na mengine. Hata hii tovuti unayoendelea kusoma ni moja ya wadau wa C2B kupitia Google AdWords na AdSense. Ukiangalia juu na pembeni mwa kurasa nyingi za tovuti utaona matangazo ya makampuni mbalimbali ambayo yanalipia hayo matangazo. Kwa maana rahisi tunawauzia huduma ya kutangaza biashara zao. Kwa hiyo mfano mimi ninayetoa mada hizi ni mtu binafsi na ninatoa huduma kwa makampuni makubwa, viwanda nk. Hapo nakamilisha maana ya C2B kwamba mtu (end user/consumer) anauza bidhaa au huduma kwa makampuni.

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content