Jinsi ya kujiunga Paypal na Skrill - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Jinsi ya kujiunga Paypal na Skrill

Jinsi ya kujiunga na mifumo ya PayPal na Moneybookers (Skrill)
Ndio, kabla hatujaangalia namna ya kujiunga na paypal au moneybookers, hebu na tuangalie pros and cons (faida na hasara) za kutumia kadi yako kwenye manunuzi mtandaoni, na kwamba paypal au moneybookers ni mkombozi wako.
  • Kwanza tambua kuwa, mtu akizifahamu namba za kadi yako anaweza kuchukua pesa zote kwenye akaunti bila ridhaa yako. Kwa kadi za visa hata mastercard kuna namba zimepangwa nne kwenye mafungu manne na zinaunda idadi ya tarakimu 16 (zinaitwa debit/credit card number) na pia zinafuatiwa na namba zingine tatu upande wa nyuma wa kadi (zinaitwa card verification code). Hizi namba ni muhimu kuzificha kila unapofanya shughuli yoyote kuhusiana na hiyo kadi yako.
  • Pili, utakwepa vipi maana ili ununue ni lazima utaingiza hizo namba zote kwenye mfumo ule unaotumika kununua bidhaa au huduma, utakwepaje sasa? Haupo salama sana kwani endapo muuzaji akiamua kukurudia atakuchukulia pesa maana tayari umeshampa details mhimu za kadi yako. Kwa wale ambao sio wenyeji wa malipo hayo tafadhali usikurupuke, soma mada isemayo Zifahamu njia salama na hatari za malipo kwenye mtandao, hapo utajifunza namna ya kufanya malipo moja kwa moja bila   kutumia paypal au moneybookers na ukabaki salama.
PayPal
Huu ni mfumo unaomilikiwa na soko la ebay, japo nimeona tangazo kuwa karibuni watatenganisha ebay na paypal. Ni mfumo uliotapakaa karibu kila soko la bidhaa au huduma mtandaoni. Taratibu za kujiunga ni kwenda kwenye tovuti yao www.paypal.com ambapo utajisajili na kupata akaunti. Kawaida yao watakata pesa kiasi cha dola moja na nusu kwa wakati huu naandika wanakata hivyo, kama utasoma maelezo haya wakati ambao imebadilika tafadhali usinihukumu. wanafanya hivyo ili kuhakiki akaunti yako na watairudisha ndani ya siku thelathini. Baada ya kukukata hicho kiwango cha pesa, watakutumia tarakimu nne kwenye statement ya akaunti yako. Ila usije ukasumbuka kwenda benki kuomba statement ukitegemea utauona huo muamala na hizo tarakimu kwenye statement yako, ni kwamba hautauona. Unaweza kuziona tu kwa njia ya internet kwa wale waliojiunga na ebanking.
Baada ua kuukamilisha huo mchakato sasa uko tayari kufanya malipo kwa njia salama kwani paypal hawatahitaji uweke namba za kadi yako kila unapotaka kununua na hawatatoa hizo namba kwa muuzaji.
Moneybookers (skrill)
Taratibu za kujiunga na moneybookers zinafanana na zile za paypal. Ingia kwenye tovuti yaowww.skrill.com na ujiunge. Tofauti na paypal ambao hukata kiwango cha pesa na kukutumia tarakimu nne, monebookers wao huchukua kiwango cha pesa na kukuuliza utaje umekatwa kiasi gani kutoka kwenye akaunti yako. Ki msingi wanataka wahakikishe kama kweli akaunti ni ya kwako maana kama sio yako hautajua kiwango gani kimekatwa.
Sasa hapa ndio utaona umuhimu wa kuwa na akaunti ya dola kwani kama unatumia akaunti ya shilingi hautajua ni dola ngapi zimekatwa hata kama utajua dola imeuzwa bei gani siku hiyo. Kwa hiyo ni muhimu kufungua akaunti ya dola na pia kujiunga na internet banking ili kukwepa usumbufu mwingine usio wa lazima. Lakini usiogope unaweza ukaachana na monebookers na ukabaki na paypal sio mbaya. Kwanza paypal ndio inatumika sana kuliko moneybookers.
Hadi hapo naamini tayari umeshafungua akaunti paypal na/au moneybookers, nakupongeza. Sasa upo salama unapokuwa ukifanya manunuzi yako mtandaoni. Sio kazi ngumu sana japo wengine inawapa shida, ukishindwa basi tupe kazi tukufanyie.

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content