Jinsi ya kulipwa kupitia Paypal - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Jinsi ya kulipwa kupitia Paypal

Jinsi ya kupokea au kulipwa pesa kupitia PayPal na Moneybookers
Paypal
·  Kama mtu atakuwa amekutumia pesa, utapata ujumbe au barua pepe yenye kusema "You've Got a Payment email."
· Kama huna akaunti ya paypal unaweza kufungua hapa. Kisha ukikamilisha kufungua akaunti, utaingia kwenye ukurasa wa paypal usemao "history". Au kama tayari unayo akaunti ya paypal basi cha kufanya ni kuingia kwenye akaunti na tafuta link hiyo hiyo ya "history" na utaona hayo malipo. Baada ya kuona kweli umepokea malipo unaweza kuziacha humo au kuzitoa.
· Kama unataka kuzihamishia kwenye akaunti yako, utakachofanya ni kuingia (log in) kwenye akaunti yako ya paypal na uangalie palipoandikwa "withdraw". Baada ya hapo utakuwa umetuma taarifa kwa mwenye kukulipa.
· Baada ya kutuma "invoice" kwa mwenye kukulipa atapokea email yenye link kisha atakamilisha malipo kutoka kwenye akaunti yake ya benki au credit/debit card. Basi hapo kama unatumia akaunti ya dola pesa itaingia moja kwa moja kwenye akaunti yako ila kama unatumia akaunti ya shIlingi bado utakuwa hujafanikiwa kuipata hiyo pesa hadi ukamilishe hatua nyingine zaidi. Hii ni kwa sababu malipo uliyolipwa ni ya dola na wewe unatumia akaunti ya shilingi, lakini usihofu hujapoteza hela, fuata hatua zifuatazo.
·Ingia (login) kwenye akaunti yako ya paypal kisha nenda kwe sehemu (tab) iliyoandikwa "history" na bonyeza (click). Baada ya hapo, pamoja na history za miamala mingine (kama ipo) utaona hayo malipo yako.
·Bonyeza huo muamala na itakuja hati maalumu ya malipo na ikiwa na namba maalumu ya hayo malipo, pili itakuwa imeonyesha Jina lako na zile namba nne za mwisho (credit card numbers) za kadi yako.
·  Baada ya kuchukua hiyo hati, sasa unatakiwa uandike barua ya kawaida au barua pepe kwenda CRDB ukidai malipo hayo yawekwe kwenye akaunti yako. Katika barua
 hiyo ambatanisha hiyo hati uliyoishusha (download and print). Pia kwenye barua utaandika majina yako kama yalivyo kwenye kadi yako (tafadhali usibadili hata
 jina moja) halafu uandike namba ya akaunti yako. Tafadhali usichanganye credit card number na account namba, hapa nazungumzia accont number yaani kwa mfano
 wateja wa CRDB ni ile iliyoandikwa 01jxxxxxxxxxx. Hiyo utaiandika kama ilivyo usiweke hizo herufi "xxxx".
· Hiyo barua ipeleke kwa mkono kwenye tawi lolote la benki na uwakabidhi kisha usubiri, utaanza kuangalia salio baada ya siku tatu (kwa uzoefu wangu). Mimi ningekushauri kukwepa usumbufu wa safari na foleni za benki, tumia barua pepe ni rahisi na pia ni njia ya haraka. Lakini pia utapata mrejesho wa kipi kinafanyika kuhusiana na hilo ombi lako. Kwa wateja wa CRDB tumia hii barua pepe kwa maulizo yote customer_hotline@crdb.com.
Hadi hapo utakuwa tayari umepata pesa yako. Lakini zingatia kuwa hayo maelezo juu ni kwa malipo yale ya kawaida mfano unatumiwa pesa na ndugu, rafiki au mtu mwingine. Kama wewe unauza bidhaa kwenye mtandao na umejipanga kupokea kwa paypal kuna njia zingine tofauti nazo zimeelezwa kwenye mada isemayo jinsi ya kuuza bidhaa au huduma kwenye mtandao. Lakini pia ni tofauti kidogo na malipo ya pesa iliyorudishwa "refund", hii pia nimeeleza kwenye mada isemayo jinsi ya kudai kurudishiwa pesa kwa njia ya paypal.

 
Moneybookers
Hapa pia mambo sio tofauti sana na paypal maana barua pepe ndio hutumiaka kupokea pesa.
·  Jambo la kwanza fungua akaunti ya moneybookers (kama huna), kama hujui jinsi ya kufungua akaunti ya moneybookers inakubidi urudi kwenye sura ya pili na ukasome    mada isemayo jinsi ya kujiunga na mifumo ya paypal na moneybookers.
· Baada ya kufungua akaunti sasa utaweza kupokea pesa kwa hatua zile kama za paypal. Unayetaka akulipe unatakiwa kumpa anuani yako ya barua pepe na akishakulipa  pesa itaingia moja kwa moja kwenye akaunti yako. Na kama unatumia akaunti ya shilingi itakubidi ufuate zile hatua nilizoeleza kwenye juu kwenye hatua za kupokea pesa  kwa njia ya paypal.
Hadi hapo utakuwa tayari unaweza kulipwa kwa njia ya mifumo ya paypal na moneybookers. Endelea kufurahia mada mbalimbali zinazofundisha namna ya kufanya manunuzi kwenye mtandao wa internet kupitia tovuti yetu hii.
 

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content