Kuuza na kutuma bidhaa nje ya nchi - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Kuuza na kutuma bidhaa nje ya nchi

Fahamu namna ya kuuza bidhaa nje ya nchi (export) ukiwa Tanzania
 
Kwanza kabisa ni vizuri upitie mada ya kwanza kabisa isemayo  Namna ya kuuza bidhaa kwa njia ya intaneti.
 
Kwa sheria ya forodha ya Tanzania haikutozi kodi ya aina yoyote wewe unayeuza bidhaa nje ya nchi isipokuwa kwa aina mbili (2) tu za bidhaa nazo ni ngozi ghafi pamoja na korosho ghafi. Endapo utakuwa unauza/safirisha ngozi ghafi toka Tanzania utatozwa ushuru usiozidi 60% ya bei ya FOB au TSH. 600 kwa kilo (kama hujui maana ya FOB inabidi usome mada isemayo Fahamu maana ya incoterms.
Na kwa upande wa korosho utatozwa ushuru usiozidi 10% ya FOB au Dola za kimarekani 160 kwa kila tani moja ya mraba (metric ton). Hivyo hadi wakati huu naandika ni bidhaa aina mbili tu zinazotozwa ushuru wa kuuzwa nchi za nje lakini bidhaa nyingine hazitozwi.
 
Hatua za kupitia unapouza/safirisha bidhaa nje ya nchi
 
·Muuzaji/msafirishaji unatakiwa kutafuta wakala wa shughuli za upokeaji na usafirishaji (Clearing and Forwarding Agent (CFA)) atakayeshughulika na maswala ya hati zinazohusika kwa njia ya intaneti.
 
·Wakala atashughulika na hati na/au vibali vyote kwa njia ya mtandao maalumu uliounganishwa kutoka kwake na mfumo wa TRA kabla ya ukaguzi wa mwisho na kutolewa kibali cha kusafirisha. Hizo ndio hatua za awali kabisa za kuzipitia unapoanza kuuza/kusafirisha nje ya nchi.
 
Hati zinazotakiwa
 
·Risiti ya mauzo
 
·Mpangilio wa ufungashaji (park list)
 
·Cheti chako cha mlipa kodi (TIN)
 
·Cheti cha ridhaa kutoka wizara husika kwa aina ya bidhaa inayosafirishwa. Mfano wizara ya kilimo kwa mazao, au wizara ya madini kama ni madini yanasafirishwa au mamlaka ya chakula na dawa kama bidhaa ni chakula au madawa.
 
·Barua ya kumruhusu au kumpa kazi huyo wakala wa upokeaji na usafirishaji (CFA).
 
Wakala atashughulikia kila mipango mwanzo hadi mwisho. Wewe kwa upande wako utakuwa na jukumu la kuwa karibu naye kwa kila hatua anayopitia ili pia uweze kutoa taarifa kwa upande wa mteja wako wa nchi ya nje mfano utatakiwa kumtumia hati ya kusafirishia toka shirika la meli (kama ni meli) au namba ya ufuatiliaji (tracking number) kama ni kwa ndege.
 

 

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content