Made in China - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Made in China

Kwa nini "Made in China" kila sehemu?
China; karakana la Ulimwengu
  • Kwa nini iwe China?
  • Kwa nini bidhaa nyingi katika masoko yote ulimwenguni zina lebo "Made in China"?
Jibu la maswali hayo sio gumu kwani hapo ulipo huenda saa uliyo nayo ni "made in China" au kiatu ulichovaa, nguo uliyovaa au hata simu ni "Made in China". Kwa hiyo wewe ni moja ya sababu ya maendeleo ya China.
Ukweli ni kwamba kwa karne hii, asilimia 80 ya bidhaa katika masoko au maduka ni "Made in China". Na sio Tanzania tu bali karibu nchi zote duniani ikiwemo Marekani ambaye ni mshindani mkuu wa ki uchumi wa China, kwa mujibu wa gazeti la China Business Daily, 2004. Nenda Kariakoo kwenye duka lolote la jumla na rejareja, shoprites na popote utakuta asilimia kubwa ya bidhaa ni "Made in China".
Kwa nini iwe China?
Ni kwa sababu ya kile kiitwacho "bei". Hii hutokana na bei rahisi ambayo viwanda vya China huwatoza wanaopeleka oda kutengenezewa bidhaa zao. Ndio maana kipindi hiki makampuni mengi duniani wanapeleka bidhaa zao kutengenezewa nchini China. Sekta binafsi na hata serikali zinapeleka kazi nyingi kutengenezewa nchini China.
Mfano wa makampuni makubwa kama Reebook, Wal-Mart, Omax ya nchini marekani yanakimbilia kuwekeza kwenye sekta ya viwanda nchini China. Leo bidhaa ndogo na kubwa zinatengenezwa China na kuuzwa duniani kote kwa bei ndogo sana. Lakini kwa kutaja kuwa viwanda vingi wanawekeza nchini China haimanishi kuwa China haina viwanda vyake inavyotumia kutengeneza bidhaa na kuuza nchini mwao na nje ya nchi.
Kuna kiwanda cha Magari kikubwa tu cha wachina wenyewe kiitwacho Wanfeng, pale utakuta gari linalofanana kwa kila kitu na Jeep Grand Cherokee inayotengenezwa Marekani na kuuzwa kwa bei isiyopungua dola za Marekani 35,000. Gari kama hilo lililotengenezwa China unakuta inauzwa dola za Marekani 10,000.
Kwa nini China iweze kutengeneza bidhaa nyingi na kwa bei rahisi?
Ni kwa sababu ya idadi kubwa sana ya watu nchini humo, hii ndio sababu ya msingi kabisa. Hadi sasa China ina wakaazi zaidi ya bilioni 1, hapo uhakika wa wafanyakazi ni wa uhakika. Na zaidi, wafanyakazi viwandani nchini China hulipwa pesa kidogo sana ukilinganisha na nchi zingine. Hata garama za mafuta vipuli na mali ghafi iko chini. Hiyo ndizo sababu kubwa kupelekea bei ya China kushuka. Maana ikiwa garama za uzalishaji zipo chini hivyo na bei ya kuuza itakuwa chini.
Changamoto kwa wachina
Chini ya chama cha kikomunisti cha CCP, wachina hawana uhuru wa matumizi ya intaneti kwa kiwango cha juu kama ilivyo kwetu. Lakini bado wanamanufaa na tekinolojia hii ya intaneti na ecommerce. Fahamu kuwa China ina ukaguzi wa kiwango cha juu kwa raia wake katika matumizi ya intaneti ukiambatana na sheria kali zinazozuia uhuru wa matumizi ya intaneti unaitwa Great Firewall.
China inao askari si chini ya 30,000 ambao kazi yao ni kusoma barua pepe zote za watu nchini humo zinazotoka na zinazoingia. Pamoja na hilo pia jeshi hilo huratibu na kufunga tovuti zote zinazoifitini serikali ya kikomunisti ya China na kuwakamata watu wote wanaotumia intaneti kuzungumza au kuishutumu serikali ya kikomunisti ya China.
Kampuni kubwa inayohusika na programu za intaneti ya Google, imekuwa ikikisaidia kikosi hiki cha China. Mfano toleo la Google la China, huwa linachuja na kuondoa tovuti na kurasa zote zenye maneno democracy na human rights .
Hata kampuni nyingine ya kimarekani Yahoo! Iliwahi kutoa ushirikiano kwa kutoa nakala za mawasiliano ya barua pepe ya mwanahabari mmoja aliyekuwa akiwasiliana na kikundi fulani cha cha wanaharakati wa kudai demokrasia cha nchini Marekani. Mwanahabari huyo alifungwa miaka 10 gerezani.
Pamoja na baraza la Congress la Marekani kuikosoa kampuni ya Google na Yahoo! Lakini bado kampuni hizi zinatoa ushirikiano kwa sheria za China.
Changamoto kwa serikali ya China ni kuwa mzigo utawalemea kulingana na uwingi wa watumiaji wa intaneti wasiopungua milioni 200 na wote wanatumia intaneti kila siku. Kitambo serikali ya China itashindwa kuratibu maswala ya barua pepe kulingana na idadi kubwa ya watumiaji nchini humo.
Darasa kwetu watanzania
Kwetu sisi Tanzania bado tunao uhuru mkubwa na matumizi ya intaneti. Basi tuzichangamkie fursa zipatikanazo katika intaneti ikiwemo ecommerce yani kuuza na kununua ili tujenge uchumi wa mtu binafsi lakini hata wa taifa kwa ujumla. Ikiwa wafanya biashara wakubwa wanatengenezea bidhaa zao China ili wapate faida, basi na sisi watanzania tunaposubiri viwanda vyetu vikue tunaweza kununua moja kwa moja kutoka China tukaokoa pesa ambayo tungeitumia kununua bidhaa hiyo hapahapa nyumbani, badala yake pesa hiyo tukaitumia kwa mahitaji mengine. Hivyo ndivyo tutakavyoweza kutoka kiuchumi pamoja na sababu zingine nyingi.
Tumekuwa tukieleza namna ya wewe msomaji kuweza kujinunulia bidhaa popote duniani kwa njia ya intaneti. Kama unasoma maelezo haya lakini hujasoma namna ya kununua kwenye intaneti, basi inakubidi usome  Elimu ya kuuza na kununua kwenye mtandao
Lakini pia huenda ukasoma mwongozo wa jinsi ya kununua kwenye mtandao na bado ukashindwa kununua wewe mwenyewe, basi nakukaribisha kwenye kampuni yetu inayojihusisha na uwakala wa kuwaagizia watu bidhaa nchi za nje hususani kwa njia ya mtandao ingia tu kwenye ukurasa wa nyumbani kisha chagua njia yoyote ya kuwasiliana nasi kuweka oda..  

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content