Malipo Salama na Hatari - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Malipo Salama na Hatari

Zifahamu njia salama na hatari za malipo kwenye mtandao
Kuna kila aina ya watu wabaya na wema katika masoko ya intaneti. Wengi hulia kwa kukosa elimu ya kutosha juu ya manunuzi kwa njia ya intaneti. Katika sura hii utafahamu namna ya kukwepa kupoteza pesa zako unapofanya manunuzi mtandaoni.
Kwanza angalia soko unalotumia kununua lina mfumo gani wa malipo? Je ni salama au si salama. Pili mwangalie muuzaji ametaja njia gani anatumia kulipwa? Ni salama au ni hatari?
Njia hatari za malipo
  • Tunaposema njia hatari tunamaanisha yale malipo ambayo yanamfikia muuzaji moja kwa moja kwenye akaunti yake kabla hajakutumia mzigo wako. Malipo hayo ni pamoja na Telegraphic Money Transfer (TT), Western Union, MoneyGram au Credid/Debit card. Malipo haya kuna uwezekano mkubwa wa kuibiwa au kutumiwa mzigo tofauti au feki, hii ni kwa sababu muuzaji ameshazipata hela sasa hana wasiwasi na hasa ukizingatia wewe upo mbali na hamfahamiani. Kwa hiyo lolote kati ya hayo   mawili anaweza kulifanya.
  • Kwa kutumia credit/debit card ni hatari pia, hasara zake zinafanana na hizo hapo juu za kutumia TT, WU au MoneyGram ila hii ina hasara nyingine mbaya zaidi. Kwa sababu ili ufanye malipo kwa njia ya credit/debit card itakubidi kuingiza namba za kadi yako, hizo namba muuzaji akizichukua anao uwezo wa kukuibia hela zote zilizomo kwenye akaunti yako. Nimeshaandika mada isemayo Jinsi ya kujiunga na mifumo ya PayPal na Moneybookers,kama hujaisoma ni muhimu uisome kwa usalama wa pesa zako.
  • Unapofanya manunuzi kwenye masoko angalia bidhaa unayotaka kununua imeandikwa inalipwa kwa njia gani, kama ameandika Paypal huyo hana wizi. Lakini kama kaandika TT, jihadhari sana unaweza kulia. Nichukue mfano alibaba ambapo sisi tuna akaunti na pia tuna uzoefu wa muda mrefu sasa. Ukikuta bidhaa kuna nembo ya "Safe Trade" huna haja ya kuwaza. Huyo ni muuzaji ambaye huitwa "verified Supplier" na hana longo longo. Safe Trade ni mfumo salama wa malipo unaotumika kwenye soko la alibaba. Unatumika kama ulivyo wa Paypal, kwamba muuzaji hapewi pesa hadi atume mzigo na alete vielelezo.
  • Kama muuzaji atakwambia usitumie Safe Trade bali tuma kwa TT au WU moja kwa moja kwake, huyo ni mwizi achana nae.
  • Kama muuzaji (hasa kwenye soko la magari la Japan liitwalo Tradecarview) akikwambia usilipe kwa kutumia "paytrade" kwa sababu hilo gari tayari lipo Tanzania, huyo pia achana nae ni mwizi. Kumbuka Tradecarview ni soko kama ilivyo alibaba, kuna mkusanyiko wa wauzaji wakiwemo wema na wabaya ndio maana wakatengeneza mfumo wa malipo kama ilivyo Paypal ambapo muuzaji hapewi hela moja kwa moja hadi alitume gari na aonyeshe documents.

 Njia salama za malipo
  • Masoko kama tradecarview, alibaba, aliexpress, ebay, amazon kwa uchache ni salama kwa sababu mifumo yao ya ulipaji ni salama mfano Paytrade kwa alibaba, alipay kwa aliexpress, Paytrade kwa Tradecarview na Paypal kwa Ebay na Amazon. Unapofanya manunuzi zingatia kulipa kutumia hiyo mifumo kwa usalama wako.
  • Pia inawezekana unanunua bidhaa au huduma kutoka kwenye tovuti binafsi, angalia pia kama anapokea malipo kwa njia ya salama. Wakati mwingine kuna wauzaji kama beforward na sbtjapan, ni wauzaji binafsi na wanapokea malipo kwa TT ila hawajawahi kulalamikiwa. Sisinwenyewe ni wateja wao ila bado TT sio salama unatakiwa ku "handle with care".
  • Inawezekana unalipa kutumia TT au WU ila sio kwenye akaunti ya muuzaji mwenyewe bali unalipa kwa Safe Trade au Paytrade. Hapo pia ni salama usiogope.

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content