Mashirika ya Usafirishaji - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Mashirika ya Usafirishaji

Fahamu kuhusu mashirika ya usafirishaji/posta: Faida na changamoto zake
Katika eCommerce, kuna bidhaa na huduma. Tunapozungumzia huduma ni kama vile unahitaji kufungua simu yako iliyofungwa na mtandao wa simu wa marekani labda AT&T au Verizon, hapo utalipia huduma ya kufunguliwa simu yako kwa kutumiwa namba za kufungulia kwa njia ya intaneti. Hivyo hapa hakuna shirika la posta litakalohusika kusafirisha hiyo huduma (nimetoa mfano mmoja kati ya mifano mingi).
Kwa upande wa bidhaa, mambo ni kinyume chake. Mashirika ya usafirishaji na posta ni wadau wakubwa wa eCommerce. Hii ndio itakuwa mada yetu kuu katika ukurasa huu. Utafahamu njia za kuweza kufikiwa na mzigo wako pale unapoununua nchi ya mbali.
Katika kununua mzigo nchi za mbali kuna njia mbili kuu za kutumia kusafirisha mzigo wako nazo ni Bahari (sea freight) na ndege (air freight). Kwa hiyo karibu kila shirika/posta lazima watumie njia moja wapo au zote mbili. Hapa chini nitajaribu kuorodhesha aina ya makampuni ambayo nina uzoefu nayo na pia tutaona faida na changamoto zake.
Hili ni shirika la usafirishaji kwa haraka  "express" na lina huduma kwa njia zote za usafiri kwa maana ya bahari, anga na nchi kavu.
Faida
 • Wanasafirisha haraka (hasa kwa mizigo ya njia ya anga). Mzigo utakaotoka Marekani, utafika Dar es Salam ndani ya siku mbili tu.
 • Wana mfumo thabiti wa namna ya kufuatilia mwenendo wa safari ya mzigo wako "tracking system". Mfano unaweza kusajili namba yako ya simu kwenye mfumo wao kwa kutumia namba ya ufuatiliaji "tracking number" na utakuwa unapewa tarifa za safari ya mzigo wako kwa kila hatua utakayokuwa unaingia au kutoka hadi utakapoupokea.
 • Huduma yao ni kukuletea mzigo wako hadi mlangoni.
 • Watawasiliana na wewe aidha kwa barua pepe au simu pale watakapohitaji maelezo fulani kama hayapo, mfano jina au TIN number wakati wa clearing (shughuli ya kutoa mzigo uwanja wa ndege/bandarini).
 • Vifaa vyao vya kubebea ni imara, wanabeba kwa uangalifu katika safari na mzigo utakufikia bila kuharibiwa.
Changamoto
 • Wanatoza gharama kubwa kwa huduma zao.
 • Kama huna TIN number itakulazimu uipate toka TRA ili zoezi la ushuru (Clearing) uwanja wa ndege/bandari liendelee.
 • Hakuna mzigo utakaopitia kwao na ukaupokea mikono mitupu hata kama ni "educational materials" ambazo hazilipiwi ushuru.
 • Hawana matawi sehemu nyingi za Tanzania na hivyo utalazimika kulipa pesa zaidi kwa ajili ya kile wanachokiita "remote fee".
 • Hawasafirishi kwenye anuani za "P.o.Box".
Ni shirika la posta la Marekani. Ni mdau mkubwa wa usafirishaji katika soko la ebay na amazon. Lina aina kadhaa za huduma ambazo ni za kawaida, kati na haraka.
Faida
 • Hawana gharama kubwa.
 • Wanatoa namba za ufuatiliaji "tracking numbers" kwa aina yoyote ya huduma.
 • Wanamuunganiko na mashirika mengine ya posta ulimwenguni likiwemo la Tanzania hivyo mzigo wako utaletwa na kukufikia kwa anuani yako ya posta (P.o.Box).
 • Vifaa vyao vya kubebea "package" ni nzuri na imara.
Changamoto
 • Hawasafirishi kwa haraka kama ilivyo DHL hata kama utachagua huduma ya haraka.
 • Pamoja na kutoa namba za ufuatiliaji lakini bado mzigo unaweza kupotea bila kujulikana upo wapi (hupotea kabla ya kufika Tanzania). Au taarifa za ufuatiliaji kwenye tovuti yao zikaishia kuonyesha safari ya mzigo nchini Marekani, baada ya hapo taarifa hamna lakini mwisho wa siku mzigo unakufikia bila taarifa. Hapo unaweza kupokea mzigo wako na ukadai haujafika na ukarudishiwa hela zako.
China Post/ HongKong post/Singapore Post
Faida
 • Hawana gharama kubwa.
 • Wanasafirisha kwenye anwani za "P.o. Box".
Changamoto
 • Hawana huduma ya haraka na mara nyingi huchelewesha sana kusafirisha mzigo wako.
 • Vifaa vya kubebea sio vizuri na imara.
 • Wanatoa namba za ufuatiliaji ila zinachukua mda mrefu kuanza kuonekana kwenye mtandao.
 • Kwa Singapore Post, hawasafirishi moja kwa moja hadi Tanzania, ni lazima watue Kenya na kuuacha hapo mzigo wako hadi utumwe tena na Posta ya Kenya. Hii husababisha ucheleweshaji zaidi.
 • Kwa ujumla wa mashirika yote haya matatu (China, HongKong na Singapore Post) ni wacheleweshaji kwani mzigo ukiwahi sana basi ni wiki nne na wakati mwingine wiki nane.
Hayo ni baadhi ya mashirika ya usafirishaji/posta ambayo ninauzoefu nayo. Najua faida na changamoto zake. Haya mashirika ukiondoa USPS, ni wadau wakubwa wa masoko ya alibaba.com, aliexpress.com, made-in-china.com na mengine kadhaa. Na unaponunua mzigo unapewa uhuru wa kuchagua shirika unalopenda kusafirishia kulingana na bajeti yako. Mara nyingi ukikuta mzigo umeandikwa "free shipping" basi fahamu kuwa utatumwa kwa moja ya hayo mashirika matatu.

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content