Masoko yasiyotuma Tanzania - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Masoko yasiyotuma Tanzania

Jinsi ya kununua/kupokea mzigo kutoka soko wasiotuma mizigo Tanzania
Kama tulivyoeleza kwenye sura nyingine juu ya aina mbili za biashara ya mtandao kwa maana ya bidhaa na huduma. Hapa pia tunazungumzia swala la bidhaa kwani huduma haina mipaka, mtu anaweza kununua programu nchini Uingereza na akaiweka kwenye komputa yake mda mfupi bila kutumia DHL wala USPS.
Kuna masoko ambayo hawatumi bidhaa moja kwa moja Tanzania, soko moja wapo maarufu ni amazon, mada hii itakuelekeza namna ya kufanya ili usikwamishwe ukashindwa kununua kwa kigezo cha anuani ya Tanzania. Tunaposema ecommerce inajumuisha bidhaa na huduma, basi hapa utakutana na mashirika ambayo yanauza huduma zao kwa njia ya intaneti. Ndio, ni huduma ya kukutumia mzigo wako pale ulipo kwa kuyatumia mashirika ya usafirishaji ambayo tumeshaangalia katika sura iliyopita.
Mashirika haya ni maarufu kwa jina la "Forwarding Companies" na mengi yapo Marekani. Moja wapo ni kama MYUS, IPS, SHIPTO na mengine. Mashirika haya (Shipping Companies) yanachokifanya ni kukupatia wewe anuani ya Marekani, yani mfano upo Mbeya Tanzania na unaitwa Mpoki Mwangumbe (mfano). Unapewa anuani labda:
     Mpoki Mwangumbe,
4299 Express Lane,
Sarasota, FL 34238 USA
Phone: 1.941.227.4444
Fax: 1.941.827.2985
      
Huo ni mfano wa anuani utakayopewa, kwa hiyo unaponunua bidhaa yako na ukifika wakati wa kutoa anuani yako, hutoi anuani ya Mbeya, Tanzania bali utawapa anuani yako ya Marekani. Mchakato wote ukikamilika, mzigo wako utatumwa Marekani badala ya kutumwa Tanzania. Mzigo utakapofika Marekani, shirika litaangalia jina la mwenye huo mzigo  wakishaliona basi haraka wanawasiliana na wewe kukutaarifu na pia kukuuliza unapenda mzigo wako wautume kwa njia gani, kwamba DHL au USPS na watakutajia garama.
Baada ya kuchagua mzigo wako utumwe kwa njia gani basi utalipia nauri au gharama za kutumiwa huo mzigo kisha watakutumia sasa kwa anuani yako ya Mbeya Tanzania.

Fahamu baadhi ya hayo mashirika hayo:
Haya tumeyataja kwa uchache kama sampuli kati ya mengine. Sisi tuna akaunti ya myus.com na ipsparcel.com, huwa wanatutumia mizigo bila shida. Namna ya kujiunga ni kuingia katika tovuti ya shirika husika kisha utajisajiri na utapewa anuani ya Marekani kama tulivyoeleza pale juu. Kujiunga ni bure kwa mashirika mengi isipokuwa kwa myus kuna ada kidogo utatoa. Myus ukijiunga nao ni wazuri zaidi kwani huweza hata kukukopesha huduma endapo hautakuwa na pesa za kutosha kwa huduma wanayokupatia.

Pili wao hupenda huduma za haraka hawataki ucheleweshaji, siku na saa ambayo mzigo wako umewafikia wanakutaarifu na wapo tayari kutuma hata siku hiyo hiyo ukitaka. Pia ili kuwahisha, hawataki kutuma kwa posta kama USPS bali hutumia sana DHL, FEDEX au UPS EXPEDITED.

Mpaka hapo twatumaini umeona jinsi dunia ilivyokuwa kijiji siku hizi, hatuzuiwi na umbali au muda na gharama, mambo mengi yanawezekana kupitia ecommerce. Endelea kusoma miongozo mingine kwa faida yako na ya taifa letu.

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content