Uza Mtandaoni - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Uza Mtandaoni

Namna ya kuuza bidhaa kwa njia ya intaneti
Pamoja na kwamba unaweza kuuza kupitia masoko yaliyopo tayari lakini bado unao uwezo wa kutengeneza soko lako mwenyewe (ila ukiamua hivyo imekupasa ujiandae vizuri kwa utaalamu wa tehama). Utatakiwa kufuata taratibu zifuatazo.
  • Kwanza nunua domain name. Hii ni anwani ya tovuti yako mfano www.kalumbilo.co.tz. Hiyo ndio domain name. Mahala pa kununua ni sehemu nyingi duniani unapoweza kununua mfano GoDaddy.com , wix.com, 000webhost.com nakadhalika. Hiyo ni mitandao ya kimataifa inayouza domain names zenye extension kama.com, .net, .org, .tv nk. Mimi ningekushauri kwa wewe mtanzania mwenzangu nunua domain name toka Tanzania na hautajuta, kwanza gharama sio kubwa na pili utakuwa na uhakika wa muda wote tovuti yako kuwa hewani. Kama utahitaji basi ingia   hapa tznic au moja kwa moja ingia hapa. Kwa kupitia hizo kampuni utapata domain name yako ya kitanzania.
  • Pili, baada ya kununua domain name utatakiwa upate web host, yani huyu ni mtoa huduma za intaneti ambaye atahusika na kurusha tovuti yako hewani. Inashauriwa aliyekuuzia domain name ndiye akuuzie na host lakini sio lazima. Unaweza kununua domain name Tanzania halafu host ukanunua USA au nchi yoyote. Mimi nakushauri pia nunua host kutoka Isp hautajuta.
  • Baada ya kununua domain na host. Hatua ya tatu sasa ni kujenga tovuti yako ya mauzo ya bidhaa unazokusudia kuuza. Kazi hii ya kujenga tovuti inahitaji wataalamu wa TEHAMA, unaweza ukawapa kazi na utawalipa kulingana na makubaliano yenu. Mimi nakushauri pia wape hiyo kazi haohao isp ambao umenunua kwao domain na host. Lakini kama utashindwa kulipia gharama za kujenga tovuti basi unaweza kutengeneza wewe mwenyewe kama unaufahamu wa TEHAMA kwa kiwango kidogo (Novice Webmaster). Kuna mifumo au programu za kujengea tovuti zinaitwa WYSIWYG (What You See Is What You Get) Interface mfano ni kama Adobe Dreamweaver, Bluegrifon, Kompozer, Nvu nk.
  • Lakini pia kuna mifumo saidizi ambayo itakufaa sana na kukurahisishia kazi unapohitaji kujenga tovuti yako. Kuna tovuti kwa  mfano Wordpress na Squarespace ambapo utachukua templates na kuzitumia kuweka namna unavyotaka kuijenga tovuti yako. Kama utashindwa njia zote hizo, basi tuwasiliane tukusaidie.
Hadi hapo sasa utakuwa tayari una uwezo wa kufanya biashara au kuuza kwa kutumia tovuti yako mwenyewe. Lakini lipo jambo jingine mhimu unatakiwa kulifanya kabla hujaenda mbele zaidi. Je una kampuni iliyosajiliwa au umesajili biashara yako? Kama bado fanya hivyo kupitia wizara ya viwanda na biashara kwenye kitengo cha Wakala wa usajili wa biashara.
Ukishasajili biashara yako nenda TRA wakakukadirie kiasi cha ushuru wako kwa mwaka kisha wakupe TIN number. Ukishapata namba ya mlipakodi TRA (TIN number) kitakachofuata uliza kuhusu Leseni. Kwa biashara za kawaida najua utatakiwa kwenda Manispaa au halmashauri ya mji ukapate leseni, kwa hii biashara ya intaneti utatakiwa kwenda BRELA ukapate Leseni hapo.

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content