Walengwa wa huduma - Njoo Tukuagizie Gari

KARIBU:  NjooTukuagizieGari MDAU

YALIYOMO
Go to content

Walengwa wa huduma

MOJA, Yapo makampuni mengi ya kuuza magari Japan na Ulaya. Mengine yanao mawakala Tanzania na mengine hayana. Ni rahisi kwenda moja kwa moja kwa wakala wa kampuni husika na kuagiza gari unayoipenda, lakini shida itaanzia pale utakapokosa gari unayoipenda katika kampuni hiyo, au ukaipata lakini ikawa juu ya bajeti yako. Itakuchukua muda na garama tena kutafuta wakala mwingine na mwingine hadi upate hitaji lako inaweza kuchukua wiki na huenda usipate hitaji lako kwa ukamilifu ila ukaamua tu sababu umechoka kuzunguka.

MBILI, kuna ulazima wa kujua na kutumia internet katika mchakato mzima wa kuagiza, kufuatilia hadi kulipata gari lako. Wapo wengi hawana ujuzi wa         internet, na wengine wanao ujuzi wa internet lakini aina ya shughuli wanazofanya zinawanyima fursa ya kufuatilia mchakato wa magari yao waliyoagiza. Kutafuta wakala wa ushuru (Clearing Agent), kulipa malipo TRA kwa iTax pamoja na mengine ni moja ya usumbufu ambao watu wanakutana nao.

TATU, wengi wetu hatuna ufahamu wa biashara ya kielektroniki (eCommerce) tukiichukulia maana ndogo lakini muhimu kwa upande wa INCOTERMS. Hatujui maana ya FOB, CIF, CIF+Inspection, CNF nakadhalika. Hii huleta usumbufu fulani na mda mwingine unaingia kwenye shida sababu hujui ni ipi INCOTERM inayotakiwa uitumie unapoingiza mzigo wako Tanzania. Mfano sheria ya kuingiza Tanzania gari iliyitumika, ni lazima ununue lenye incoterm ya CIF+INSPECTION. Tofauti na hapo utapigwa faini ya asilimia 30 ya pesa yote uliyogharamia na bado utalazimika kulipeleka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) likakaguliwe, kule hutoki kama ni bovu lazima itakugarimu kulitengeneza na bora uombe liwe na ubovu mdogo, vinginevyo unaweza kulitelekeza.

Sasa hayo yote, sisi ndo tupo kusaidia. Kwa yeyote ambaye hahitaji usumbufu wowote anakuja kwetu, UKIJA KWETU UTAKUWA UMEYAFIKIA MAKAMPUNI YOTE YA JAPAN NA ULAYA, na utachagua gari ukilinganisha kwa makampuni yote tukiwa katika meza moja, hivyo utaepuka usumbufu wa kuzunguka huko na huko.

Ukitupa kazi sisi tutafanya kila kitu kwa niaba yako, usumbufu wa kila aina tunaubeba sisi na mwisho tutakuita tu uje upokee gari lako lipo tayari kuingia barabarani. Malipo yetu ni 10% ya CIF [Inajadiliwa] hiyo ndiyo riziki yetu tunayopata kwa kazi utakayotupa. Mfano kama gari imelipiwa japan mil 5, basi ya kwetu ni laki 5. Muda mwingi mteja wetu halipi hiyo 10% lakini muuzaji wa Japan anatupa yeye kupitia punguzo kwani tumekuwa mawakala wao. Ndiyo maana tutakuhudumia na bado bei itakuwa chini ukilinganisha na kununua showroom.

Jambo la kuzingatia ni hili, kama unahitaji gari lako haraka tunakushauri nenda showroom ukanununue, zipo gari nzuri na wauzaji wapo wazuri kabisa na hata ukihitaji tukuelekeze walipo tutakuelekeza na tumekuwa tukifanya hivyo mda wote. Bei utakayonunua ni lazima iwe juu sababu huyo auzaye naye amenunua Japan, analipa wafanyakazi, analipa ushuru, na garama zingine za uendeshaji na mwisho wa siku anataka faida.

Lakini kama upo tayari kusubiri muda wa mwezi na nusu, basi agiza wewe mwenyewe au kipitia kwetu na utakuwa umeokoa kiasi kikubwa tu cha pesa. Siku zote tumekuwa tukiwambia wateja wetu kwamba, KAMA KIPAUMBELE CHAKO NI KUOKOA MUDA BASI GHARAMIA PESA ZAIDI na KAMA KIPAUMBELE CHAKO NI KUOKOA PESA ZAIDI BASI GHARAMIA MUDA WA KUSUBIRI.

Kwa hiyo kipaumbele chako ndo kitaamua uwe mteja wetu au vinginevyo.
Tumehudumia wengi hadi sasa, na wanashukuru na wengi wamekuwa mashahidi wetu kwani wanatutangaza vizuri na wateja wapya wanakuja kwa kuelekezwa na hawa tuliowahudumia. Tunakukaribisha wewe pia ambaye utaona huduma yetu inakufaa.

MAKAO MAKUU

Quality Plaza, 2nd Floor, West Wing, Room No. 346
Nyerere Road, Dar es Salaam
S.L.P 100047
+255 684 454 441
+255 713 416 275
www.kalumbilo.co.tz

            Mawasiliano ya haraka
Whatsapp na Barua pepe
Za jumla [General] 0713 416 275
                                     0684 454 441
          Mwanza Pekee:     0767 251 237
          Mbeya Pekee:       0629 822 276


Email:  service@kalumbilo.co.tz
© 2015-2020 Kalumbilo Imports & Commission Agency Co. Ltd  
Back to content